Jumamosi, 5 Novemba 2016

 MamboYakuzingatia Unapotaka Kununua Simu

Siku hizi kumekua na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za mkononi, na nyingi zikiwa Smart phones ambazo hutumiwa sana na vijana lakini pia rika mbali mbali, lakini Rozzie magazine inakuongoza katika vitu vya msingi vya kuzingatia kabla hujanunua smart phone yako

Uwezo wa Kamera

Kamera ni kitu cha msingi sana kwenye uchaguzi wa simu siku hizi. Umuhimu wake umekuzwa na matumizi ya mitandao ya jamii ambayo imeleta urahisi wa kusambaza picha hizo kwa watu wetu wa karibu. Kipimo kirahisi cha ubora wa kamera kinachotumika ni ukubwa wa Mega-pixels ila kuna vipimo vingine muhimu zaidi kama ubora wa lens, ubora wa sens, ambayo ndio inayopokea picha na suala la ‘image stabilization technology’ ambayo inapunguza ubovu wa picha kutokana na kutingisha mkono.

Uhifadhi (Storage Capacity)

Simu nyingi zina uwezo wa kupokea memory cards ili kuongeza hifadhi ila ukubwa wa hifadhi ya ndani ya simu ni muhimu zaidi, kwani unakuonesha uhuru wako wa kushusha programs na mara ngapi utahitaji kufuta au kuhamisha vitu kutoka kwenye simu yako.
Kama wewe ni mtu wa kutumia apps nyingi na unapenda uhuru huo, epuka simu zenye hifadhi ya ndani chini kama 4GB.

Kumbukumbu/RAM

RAM imekuwa maarufu kwenye computers lakini hivi sasa smart phones zimekuja na hizi RAM ambazo ni Kumbukumbu ni moja ya mambo yanayobana kasi ya simu yako kwenye kuendesha programs
Katika soko la sasa, RAM ya 512 – 800MB utaipata hadi Tsh 200, 000.RAM ya uhakika ya 1GB inapatikana kwenye simu za bei ya kati inayoambaa-ambaa hadi Tsh 600, 000. RAM ya 2GB+ ni bora zaidi na inapatikana kwenye simu za hali ya juu kama Samsung Note na Nexus 6. Apple i-phone 6 ina kumbukumbu ya 1GB na simu za Windows huwa na RAM ndogo pia kwa kuwa hutumia kumbukumbu kidogo zaidi ya mfumo wa Android

Processor

Prosesa ni sehemu muhimu inayobana mambo mengi ikiwemo jinsi simu inavyomudu rangi, chaji ya betri na kasi ya kuendesha program. Processor zinapambanishwa kwa kipimo cha GHz, ambapo namba kubwa zaidi inaonesha uwezo mkubwa na kasi zaidi.
. Inafaa ulize ipi inayotamba sokoni kila wakati kwa sababu zinatengenezwa kwa kasi sana.

Betri na Chaji

Teknolojia ya betri inatabiriwa na baadhi ya watu wa teknolojia kukuwa kidogo sana licha ya jitihada za karibuni zilizotoa betri zilizopungua ukubwa na zinazochaji haraka, na hata kuongeza usalama wa hizi betri.
Unaponunua simu angalia uwezo wa kukaa na chaji(unaopimwa kwa mAh) na teknolojia ya betri. Betri za mhA 2000 na kuendelea zitakupa muda kuanzia masaa sita ya chaji ukiwa unaitumia simu sana. Chini ya hapo unahitaji uvumilivu wa kutosha wa kutembea na chaja au betri ya ziada au kujibanana.

Mfumo-endeshaji (Os)

Kwa sasa, soko limetawaliwa na Android, IOS na Windows huku BlackberryOS na mifumo mingine ikijitahidi kubaki.
Windows inasifiwa kwa kutengenezwa vizuri (‘hardware build’), Android inasifiwa kwa uhuru wa kuifanya utakavyo na kubadilisha muonekano wake utakavyo. Simu za Apple zinasifiwa kwa kuwa na kiwango na mvuto wa kipekee. Blackberry yenyewe inapendwa na wafuasi wake kwa sababu ya kibodi yake na upekee wa aina yake.

Ukubwa na Uhalisia wa Screen

Screen bomba kwa sasa ni yoyote yenye ukubwa wa kuanzia inchi 4.5! Hili ni kutokana na wachambuzi wengi na hata ukiiangalia simu zinazoingia sokoni sasa hivi. Watu wanataka kuona kioo kikubwa, siyo kuchungulia skrini tena.
Kama unapenda rangi na uhalisia na pia kudumu, screen bomba kabisa zinapatikana kuanzia laki 3.5 kwa simu ya S3, kwa sasa, ila chini ya hapo, hamna tofauti sana..

Hitimisho

Moja ya vitu utakavyosikia kutoka kwa muuzaji ni, ‘Simu hii ina whatsapp.’ Ila wanchokosea ni swali hili: Unataka kuitumia simu yako mpya katika mazingira gani na unataka uhuru wa aina gani?
Kama ni mtu wa kazi, unahitaji simu yenye kasi na inayokutambulisha. Kwenye mazingira ya kimasomo, unataka simu inayokupa uhuru wa kiuchumi. Kama ni mtu wa nyumbani au mtandaoni, unataka simu yenye mfumo unaokupa uhuru wa starehe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni