Jumatano, 9 Novemba 2016

Jinsi Ya Kufanya Betri Ya Simu Kukaa Muda Mrefu !!

Tuna tumia simu zetu kufanya vitu vingi sana kucheza games, kutuma na kupokea e-mails, kununua vitu, kupiga picha, kurekodi video na hata kupiga simu (ndio bado watu wanafanya hivyo). Sasa bila simu zetu 
maisha kidogo yangezidi kuwa magumu sanasana  pale betri inapoishiwa chaji na simu kuzima wakati bado una matumizi na hiyo simu. Kwa ujumla Njia ya kupunguza
uishaji wa betri ni kuzima vitu vyote katika 'smartphone' yako ambavyo vinaifanya hiyo simu iwe 'smart' Lakini kwanini upitie yote hayo?
Zifuatazo Ni Njia Za Kuongeza Uhai Wa Betri La 'Smartphone' Yako

1. Zima 
hapana sio simu yako bali ni yale mambo yote ambayo hutumii kwa wakati huo. kwa mfano kama uliwasha 'Bluetooth' inabidi uizime hata WiFi , GPS services, Widgets, Location vyote vinabidi vizimwe kama havitumiki. chukua mda wako pitia 'settings' za simu na ufanye hayo yote 

JINSI:  nenda katika iOS settings au Andoid  settings ili kuzima hivi vitu vyote 

2. Fifisha Mwangaza
Inaweza kukushangaza kuwa kitu kikubwa kinachomaliza betri katika simu yako ni 'screen'  kwasababu inatumia 'power' nyingi  hapa kitu cha kufanya ni kupunguza mwangaza wa hiyo simu pia kuifanya iwe inatoa mwangaza 'automatically'

JINSI:  iOs Settings > Wallpaper & Brightness. Android Settings > Display > Brightness 

3. Zima Mngurumo
hapa ndipo watu wengi wasipojua, simu inatumia umeme mwingi inaponguruma kuliko pale inapotoa sauti. hivyo basi inabidi mingurumo yote isiyo ya lazima izimwe 

JINSI: iOs Settings > Sounds.  Android Settings > Sounds & Display > Phone Vibrate 

4. Epuka Wallpaper Zinazobadilikabadilika 
Hizi Wallpaper zinaonekana nzuri pia zinavutia na kupendezesha simu laki zinamaliza betri sana kuliko wallpaper ambazo hazibadiliki hivyo inabidi ziepukwe 

JINSI: iOs Settings > General > Accessibility >Reduce motion > ON.  Android Settings > Sound & Display > Animation 

5. Epuka simu Kufanya Automatic "App Updates' 
Hii inasaidia betri kutoisha mapema tena hasa kama una app nyingi katika simu yako.Sababu usipozima simu itakua kila wakati inaangalia kama kuna update ya app yoyote kisha ifanye kuiupdate (download)

JINSI: iOs App Store > Updates .  Android Google Play Store  > My Apps

Kama Bado Tatizo halijapungua kuna Njia Ya Jumla Ya Kupungunza Nayo Ni

 A: Kwa iOs Tuu

watumiaji wa iphone ambao wanatumia iOs 7 wana vitu vingi ambavyo vinamaliza betri ya simu lakini pia vinaweza vikazimwa . kwanza Nenda katika  Settings > General > Accessibility > turning Reduce Motion > ON hii itazuia kucheza cheza kwa mafile pale unapoyafungua . Pia  Settings > General > Background App Refresh kisha uzime kila App ambayo huitumii 

B: Kwa Android Tuu

Watumiaji wa Android wana njia nzuri ya kujua ni App gani inatumia Betri sana Njia ni kwenda Settings > About Phone > Battery Use ili kuona ni App gani inatumia betri sana kuliko zingine na kama ni kitu ambacho kweli hutaki kukiondoa au kukizima njia mbadala ni ku 'download'  juice defender Hii App itafanya vitu vyote ambavyo ungefanya ili kuongeza uhai wa betri lako  'automatically'  mfano kuzima Bluetooth na WiFi kipindi hauvihitaji

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni