Ijumaa, 4 Novemba 2016

Jinsi ya kuflash simu zenye MediaTek chipset
naamini clone zote zinatumia mtk pia nahisi hata za tecno nazo zina hii chipset

1. anza kwa kuandaa mazingira ya kuflash simu yako ambayo labda iko bricked, au ina tatizo lolote kama hii yangu iliyokuwa inajirestart muda wote

vitu unavyohitaji ni
a.) drivers za simu (kama chip yako ni MT65xx family download hapa) na 
b.) Smart Phone flash tool download hapa
c.) Mtk Droid Tools download hapa
d.) ROM / firmware ya simu yako (hakikisha ni rom sahihi kwa model ya simu yako) Rom karibia zote zinapatikana hapa

2. Tuanze sasa
a.) chomeka simu yako na iache ifanye installation ya driver zote, kama zingua install driver hapo juu(kama simu yako ni mt65xx)
b.)kwa sababu simu za clone hazijulikani model maana zina imitate original, basi tutatumia MTK droid tool kujua model ya simu yetu. fungua application na uiache italeta details zote kuhusu simu

[​IMG]

c.) tayari taarifa za simu tumezipata , kinachofuata hapo ni kudownload firmware specific kwa ajili ya simu yetu. ROM/firmware zipo hapa (ili kudownload inabidi ujisajili kwanza) pia unaweza kugoogle utapata tu. hakikisha una extract na ndani kuwe na faili MT(model ya simu yako)_Android_scatter.txt (hakikisha kuna neno scatter kwenye jina la hili file)

d.) hapo sasa kila kitu tunacho tunaweza kuanza kuflash simu yetu...
i. ichomoe simu, kisha fungua SP flash flash tools, sehemu ya scatter-loading file weka lile .txt file nililokwambia limo kwenye folder uliloextract kule juu

pia nenda options > usb mode iwe ticked pia hapohapo kwenye options angalia DA download all > Speed > force high speed inakuwa checked

[​IMG]

ii. click download kisha iache (usichomeke simu kwanza mpaka imalize) ikimaliza chomeka simu bila betri ukisikia mlio wa simu imekuwa connected kwenye pc haraka rudisha betri bonyeza "firmware -> upgrade" kisha tulia itaanza kuflash simu

ii. kama kila kitu kimeenda sawa utaona progress kwa rangi ya njano kama kuna makosa itatokea rangi nyekundu na maelezo 

[​IMG]

ikikamilisha successiful, itaonesha kiduara cha kijani

[​IMG]


hapo sasa unaweza chomoa simu yako na kuiwasha na utaona inaanza kama mpya vile....



ukipenda unaweza kuiroot, kubadili IMEI, kuondoa application za kichina zote kwa kutumia MTK Droid tools

       KUMBUJKA; sitausika kama utaalibu simu yako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni