Jumapili, 13 Novemba 2016

Tumeona mafanikio ya Android katika kuteka soko kubwa la simu, Android ambayo ni jamii ya 'Operating System' za linux iliingia sokoni kupitia simu ya HTC Dream mwishoni wa mwaka 2008 na hadi mwaka huu ndo inaongoza kwa umiliki wa soko duniani ikitumiwa na kampuni mbalimbali kubwa za simu kama Samsung, HTC, Motorola na Huawei.

Na sasa Mozilla Foundation watengenezaji wa kivinjari cha Firefox nao wapo katika harakati za utengenezaji wa 'operating system' kwa ajili ya kutumika kwenye simu kama vile Android. OS hii itajengwa kwa kutumia lugha ya HTML5.



Mozilla kupitia blogu yao waleeleza kupata kuungwa mkono na mashirika mbalimbali duniani hasa yakiongozwa na makampuni yanayohusika na sekta ya mawasiliano. Mashirika haya ni pamoja na Deutsche Telekom, Etisalat, Smart, Sprint, Telecom Italia, Telefónica na Telenor.


HTC Dream: Simu ya Kwanza Ya Android Sokoni
Pia makampuni yanayojihusisha na utengenezaji na simu,  TCL Communication Technology(Alcatel) na ZTE yamesema yatakuwa tayari kuteneza simu zinazotumia 'operating system' ya Firefox 0S. 

Simu za kwanza zitakazokuwa zinatumia Firefox OS zinategemewa kuuzwa katika soko la Brazil mwanzoni  mwa mwaka 2013. 

Je simu za Firefox OS zitaweza kuliteka soko kama Android OS ilivyofanikiwa? Majibu tutayapata, kwa sasa tusibirie habari zaidi za maendeleo ya Firefox OS hapa hapa Teknokona!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni