Jumatano, 2 Novemba 2016

Watanzania wengi zaidi wanajiunga Instagram kwa sasa, hivyo nimeona ni muhimu kuandika kuhusu kitu kipya kilichoongezwa katika toleo (update) jipya la app yao liliotoka siku chache zilizopita. Tolea hilo la 3.5, limeleta uwezo wa kuwatagi ('tagging') marafiki zako kama unavyoweza fanya Facebook.



"Kwa wale ambao hawaifahamu, Instagram ni mtandao wa kijamii unaohusisha watu kutuma picha ukiwa na uhuru wa kuweza kuzibadilisha muonekano kabla ya kuituma ('post') kwa ukurasa (profile) wako. Instagram inatumia mfumo wa marafiki kama wa Twitter ambapo mtumiaji badala ya kuomba urafiki anachagua kufuatilia picha za watu anaopendelea yeye bila wao kuwa na ulazima wa kumfuatilia yeye."
Kama rafiki yako akikutagi basi picha hiyo itatokea kwenye picha za kwenye ukurasa wako pia. Hivyo itaonekana kwa wanaokufuatilia wewe ('Followers). Katika toleo hili la 3.5 wameongeza kitu katika sehemu ya 'profile' yako ili kukuwezesha kuziona picha ambazo marafiki na watu wengine wamekutagi.


Kabla ya Toleo Jipya
Baada ya Toleo Jipya, Sehemu ya Mwisho ndiyo ya 'Photos of You'

MUHIMU: Kama ungependelea uwe unapitia na kuzikubali picha ambazo watu watakutagi kabla hazijaingizwa kwenye profile yako basi fuata maelekezo haya.

Nenda sehemu ya 'Photos of You', kisha nenda kwenye kisehemu cha 'Settings' kisha badilisha mfumo wa uchaguzi(selection) kutoka “Add Automatically” kwenda “Add Manually.” Kuanzia sasa kabla picha haijajumuishwa kwenye picha zako itabidi uzikubali kwanza

    Usisahau kuweka maoni yako

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni