Jumapili, 30 Oktoba 2016

Usiteseke Tena Na Anti virus Wasio Fanya Kazi Kwenye Compyuta Yako. Tumia Hawa Sasa Nibure Tu.

Kuilinda computrer yako dhidi ya virus ni jambo muhimu. Na katika kuilinda hiyo computrer unaweza ukanunua ant virus au ukaamua kutumia 'free ant virus'.  Kama utakua na uwezo wa kununua basi ni vizuri ukafanya hivyo kwa usalama wa data za computrer yako dhidi ya virusi ila kama utashindwa kununua basi hizi zifuatazo ni ant virus ambazo hutolewa bure:-
AVG
Hii hutolewa bure ikiwa na uwezo wa kuji-update yenyewe automatically au kwa kuruhusu mwenyewe
AVAST
Hutumika kwenye operating system ya windows pia huweza kuji-update. Hii pia ina uwezo wa kuchuja vitu kwenye internet na kurusu vitu ambavyo ni salama kwa compyuta yako. Pia hii huja na ulinzi wa email, chat pamoja na P2P.
Antivir
Hii wakati mwingine huitwa avira. Hupatikana katika operating system za Windows XP, Windows Vista, Windows 7, Windows 8 na Linux/Unix. Hupatkana bure kwa matumizi binafsi. Pia huja na uwezo wa kulinda computer kutokana na vitu unavyopakua (unavyo-download). Pia huweza kujiupdate automatically.
Microsoft security Essential
Hii kwenye window8 huitwa Window Defender. Hulinda computer kutokana na virusi,spyware na vitu vingine vya kudhuru computer. Hii ni ya bure na hupatikana kwenye website ya microsoft wenyewe. Pia huji update yenyewe yenyewe na hutoa onyo pale ambapo kuna shambulio la kompyuta

KAMA UNATUMIA SIMU YA SAMSANG ‘GALAXY NOTE 7’, ACHA SASA KWASABABU ZINA TATIZO LA KULIPUKA KWENYE CHAJI.

Kufuatia ripoti za matukio mengi ya watumiaji wa simu za Samsung kulipukiwa na simu hizo wakati wa kuchaji, kampuni hiyo ya Kikorea hatimaye imewataka watumiaje wake kutupa toleo la ‘Galaxy Note 7’ kutokana na tatizo hilo.

Kampuni ya Samsung imetoa tamko rasmi kupitia tovuti yake ikiwataka watumiaji wa simu hizo toleo la ‘Galaxy Note 7’ duniani kote kuchukua tahadhari na kuacha kabisa kuzitumia  wakati ikiendelea na uchunguzi zaidi.

“Tunafanya kazi na Mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusu kuwepo kwa ripoti za matukio yanayohusu Galaxy Note7. Kwa sabababu usalama wa mteja wetu ni kipaumbele, Samsung tunawataka wauzaji wote wa simu zetu duniani kuacha mara moja kuuza Galaxy Note 7,” imeeleza taarifa rasmi ya kampuni hiyo.

Majaribio ya betri ya simu ya Samsung, Galaxy Note 7 yaliyofanywa katika maabara moja nchini Singapore yalipelekea simu hiyo kulipuka moto.

Hivi karibuni, hata hapa Tanzania, kumekuwa na ripoti za matukio ya wananchi wengi kudai kuwa wameripukiwa na simu za Sumsung walipokuwa wanachaji. 

Pia, kulikuwa na taarifa ambazo hazikuthitishwa na Mamlaka kuhusu watu kulipukiwa na simu hizo walipozipokea wakati zikiwa kwenye chaji.

JIfunze jinsi ya kutafsiri ndoto uliyoota

Katika Uislamu tumeambiwa Ndoto ni sehemu ya unabii tulioachiwa, pia uislamu unaeleza aina kuu mbili za ndoto yaani Ndoto zinazotokana na shetani na ndoto inayotoka kwa mwenyezi mungu. 

Pia Uislamu umeeleza ndoto ya kweli uotwa muda gani (Mfano amesema bwana Mtume, ndoto yeyote atakayeota muumini kabla ya swala ya alfajiri, ndoto hiyo ni ya kweli), kwa ufupi ndoto ya kweli ni ile mtu anayeota usiku wa manane akiwa hana msongamano wa mawazo na hajalala na janaba.

Uislamu umesema kuwa kama mmoja wenu ameota ndoto nzuri basi amfuate mmoja wenu anayejua na amweleze ili apate maana yake. Kama uislamu umeelezea vizuri kuhusu ndoto Je ndoto hutafsiriwaje?..

Kwa ufupi kuna watu wengi wanadai wana uwezo wa kutafsiri ndoto, ukweli ni kuwa utafsiri wa ndoto ni ngumu sana na hakuna mtu anyejua kutafsiri ndoto zote ukiondoa manabii ambao kwa sasa hawapo tena. Wengi wanaishia kudanganya maana halisi ya ndoto, kumbuka uislamu umesema, "KAMA MMOJA WENU AKIOTA NDOTO CHAFU NA MBAYA BASI ASIITANGAZE, MAANA NDOTO HIZO ZIMETOKA KWA SHETANI".

Leo nitawafundisha jinsi ya kutafsiri ndoto ili msije mkadanganywa na mtu lakini tafsiri nitakayowapa ni Based on Islam na sio dini nyingine, japokuwa baadhi ya ndoto inabeba maana sawa kwa muislamu na siye muislamu. Kama wanavyotafsiri wanazuoni wengine..

Ukiota ndoto yoyote katika wakati ulioelezwa basi angalia hiyo ndoto kama inafanana na Aya yeyote ya Kuran anu Hadith Yeyote ya Bwana Mtume PBUH. Hiyo itakuwa ndio maana yake:-

Mfano 1: Umeota umetumbukizwa kwenye Kisima, tafsiri yake ni surat Yusuf... Yaani Ndugu zako wanataka kukutendea uadui, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi mungu hawatafanikiwa wanavyotaka na utakuja kuwa na uwezo wa mali na mamlaka kuliko wao.

Mfano wa Pili: Umeota ndege amekudondoshea jiwe kichwani, Tafsiri yake Surat fil... Unaonywa kuwa unafanya yaliyovuka mipaka hivyo utaangamia.

Mfano wa tatu: 
Umeota Ndege anaokuambia kitu, Tafsiri yake ni surat Naml.. Habari anayokuambia ni ya kweli hivyo unatakiwa uifanyie kazi haraka.

Mfano wa nne: Umeota unakurupuka na ukaambiwa kiama!, watu wengi wanakwenda wasipopajua, Tafsiri yake ni kuwa unapewa Onyo kuna jambo linalomchukiza Mungu unalifanya acha mara moja. kumbuka pale allah aliposema kuwaambia waovu "Hakuna wanachokisubiri ila ni kiama ambacho kitawakuta Ghafla".

Inshaallah nisiwaboe kusoma ila hivyo ndivyo jinsi ya kutafsiri ndoto.... Kesho nitawaelezea maana ya kuota manabii... Ingawa kizazi cha sasa imekuwa ngumu sana mtu kuota nabiii yeyote yule..

Jifunze Jinsi Ya Kuishinda Hofu Ya Kupata Hasara Kwenye Biashara Yako.

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA  karibu tena kwenye kipengele chetu cha kujadili changamoto zinazotuzuia kufikia mafanikio. Leo katika kipengele hiki tutajadili jinsi ya kuishinda hofu ya kuana biashara.
Watu wengi wamekuwa na mawazo mazuri ya kuanzisha biashara ila inapofika kwenye kuanza utekeleaji wa mawazo yenyewe wanakutana na hofu ambayo inawazuia kuanza. Inawezekana hata wewe umeshindwa kuanzisha biashara yako au kuikuza zaidi kutokana na hofu. Sio lazima hofu hii iwe moja kwa moja, baadhi ya watu hutumia sababu nyingine kama ukosefu wa mtaji au kutokujua biashara nzuri kama kisingizio cha kuficha hofu yako.
Kabla hatujaangalia jinsi ya kuepuka hofu hii ya kuanza biashara, tuone maoni ya msomaji mwenzetu;
Changamoto kubwa inayonikabili ni uoga wa kujaribu kufanya jambo fulani hasa biashara nikihofu kuwa naweza pata hasara na pesa yangu ikawa imeishia katika hasara hiyo.
Unakuta nakuwa na wazo zuri la kuanzisha biashara lakini uoga ndo unaonimaliza nguvu.
Je utanisaidiaje kuepuka uoga ili nisonge mbele???
Kiufupi, mi ni mwajiriwa wa kampuni moja kubwa hapa nchini.
Kama tulivyoona changamoto ya msomaji mwenzetu, yeye anashindwa kuanza biashara kwa kuhofu kwamba anawea kupata hasara. Kupata hasara ni hofu ambayo inawazuia watu wengi sana kuingia kwenye biashara. Hata wale ambao tayari wako kwenye biashara hofu hii inawazuia kutanuka na kukua zaidi.
Ni kweli kwamba kuanzisha biashara yoyote ni kitu cha hatari sana, hii ni kwa sababu kuna vitu vingi sana ambavyo huna uhakika. Na biashara yoyote mpya ina hatari kubwa ya kushindwa kuliko ilivyo na uwezekano wa kufanikiwa. Lakini hofu hii haipaswi kutufanya tusianzishe au kukuza biashara zetu.

Njia za kuepuka hofu ya kupata hasara kwenye biashara.

Zifuatazo ni njia ambazo unaweza kuzitumia kuishinda hofu ya kupata hasara unapoanzisha biashara.
1. Angalia wafanyabiashara waliofanikiwa na jifunze kutoka kwao.
Wafanyabiashara waliofanikiwa wana uzoefu mkubwa sana kwenye biashara wanazofanya. Watu hawa wameshafanya makosa mengi sana na hivyo wanaweza kukusaidia usirudie makosa ambayo yaliwapatia wafanyabiashara hao hasara. Unaweza kuwatafuta na kujifunza kutoka kwao na kama huwezi kuwapata watu wa aina hii soma vitabu vinavyoelezea mafanikio ya wafanyabiashara wakubwa. Hii itakupa mbinu walizotumia wao na pia itakupa moyo pale utapoona kwamba pamoja na mafanikio makubwa waliyonayo waliwahi kupitia kushindwa.
2. Fanyia utafiti wazo lako la biashara.
Kitu kingine kikubwa kinachokufanya uwe na hofu kubwa ya kuanza biashara ni kutokuwa na uhakika na wazo lako la biashara. Hivyo chukua muda wako na fanya utafiti wa kutosha kwenye wazo lako la biashara. Angalia utofauti wa wazo lako na mawazo ya wengine na ambalia ubunifu ambao unaweza kuuweka na kuifanya biashara yako kuwa ya kipekee. Pia angalia changamoto zinazoweza kulikumba wazo hilo la biashara na kujipanga jinsi ya kujikwamua ikitokea changamoto hizo zimetokea.
3. Anza kidogo.
Pamoja na kujifunza kwa waliofanikiwa na hata kufanya utafiti wa wazo lako la biashara, bado hofu ya kushindwa ni kubwa. Hivyo ili kuishinda hofu hii anza biashara yako kwa hatua ndogo ndogo. Hata kama una wazo kubwa la biashara, anza kidogo, angalia hatua ndogo unazoweza kuanzia kisha anza hapo. Tumia sehemu ndogo ya mtaji kuingia kwenye biashara hiyo na jifunze kwa kila hatua unayopiga. Kwa njia hii utajua ni sehemu gani inaweza kukuletea faida kubwa na pia ni sehemu gani yenye changamoto nyingi na hivyo kuhitaji umakini zaidi. Unaposhindwa kidogo inakupa wakati mzuri wa kufanya marekebisho kuliko ambavyo ungeweka mtaji wote na ukaishia kuondoka kwenye biashara.
4. Zungukwa na watu ambao wana ujasiri kwenye biashara.
Kama bado wewe ni muajiriwa na una mpango wa kuanzisha biashara, ukijadili mpango wako huu na wafanyakazi wenzako watakuogopesha sana. Watakupa maneno mengi ya kukutisha, watakwambia huwezi, watakupa mifano ya waliojaribu na wakashindwa na hivyo utakubaliana nao na kuachana na mawazo yako ya kuanzisha biashara. Kitu muhimu wewe kufanya ni kutafuta njia ya kuwa karibu na wafanyabiashara au watu ambao wana ujasiri wa kushinda hofu ya kupata hasara. Tafuta kikundi cha wafanyabiashara na kuwa nao, hawa watakupa moyo wa kuanza na pia watakushauri pale ambapo utakutana na changamoto.
Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA jiunge sasa kwa uanachama wa GOLD na utapata nafasi nzuri ya kukutana na watu ambao wameweza kushinda hofu kwa namna moja au nyingine.
5. Jua kwamba haupo mwenyewe na dawa ya hofu ni kuanza.
Njia nyingine unayoweza kutumia kushinda hofu yako ya kupata hasara ni kujua kwamba hauko mwenyewe. Kila mtu unayemuona ana hofu zake, kila mafanyabiashara unayemuona haijalishi ana mafanikio kiasi gani naye ana hofu zake. Kinachomtofautisha yeye na wewe ni ule ujasiri wa kuanza na kujifunza kadiri anavyopiga hatua. Hivyo kwa vyovyote vile anza, wanasema dawa ya hofu ni kufanya kile unachohofia kufanya na hofu hufa yenyewe. Kama tulivyosema hapo juu, anza kidogo, anza chochote kinachohusiana na biashara unayotaka kufanya, kidogo kidogo utaona unaanza kupata ujasiri na kuishinda hofu uliyokuwa nayo mwanzo.
Mwisho kabisa kumbuka kwamba hakuna kitu unachoweza kufanyakikakuondolea kabisa hatari ya kushindwa, hakuna. Maisha yenyewe ni hatari, sasa hivi umeajiriwa lakini unaweza kushangaa kesho ajira yako ikaisha, lakini hii haijakuzuia kuendelea na ajira. Unaweza ukapanda gari na mbele likapata ajali na hata ukafa, lakini hiyo haikuzuii kupanda gari. Hivyo hivyo unaweza kuanza biashara na ikapata hasara, lakini hii isikuzuie wewe kuanza biashara. Kila kitu kwenye maisha yetu kina hatari ya kutoweka bila ya sisi wenyewe kujua. Hivyo fanya kile ambacho unafikiria kufanya, huku ukijifunza na kurekebisha kadiri unavyokwenda.
Kauli mbiu yetu kwa mwaka huu 2015 ni kama NIKE wanavyosema, JUST DO IT, CHOCHOTE UNACHOTAKA KUFANYA WEWE ANZA KUFANYA, kama kuna kitakachotokea baadae utajifunza na kufanya marekebisho. Kukaa tu na kuhofu hakutakusaidia chochote

SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016 JIJINI MWANZA KUWA BORA ZAIDI

Leo Oktoba 19, 2016 Kamati ya Shindano la Maandalizi ya Miss Tanzania 2016 imesema Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29,10, 2016 katika viunga vya Rock City Jijini Mwanza, litakuwa bora zaidi kutokana na maandalizi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika.

Na BMG
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hashim Lundenga (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Rhino Agency inayoandaa Miss Tanzania, amesema baada ya mashindano hayo kufanyika Jijini Dar es salaam miaka yote, kamati hiyo imeamua yafanyike Jijini Mwanza na kwamba yatafanyika kwa miaka mitano mfululizo.
Amesema washiriki wote 30 katika shindano hilo ni bora hivyo yeyote atakayeibuka mshindi ataliwakilisha vyema taifa kwenye mashindano ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika Disemba 18, 2016 Jijini Washingtone DC nchini Marekani.
Viingilio katika shindano hilo ni shilingi 20,000, 50,000 na 100,000 ambapo inategemewa kwamba wasanii Ali Kiba pamoja na Christian Bella ikiwa wataafiki makubaliano watadondosha burudani katika shindano hilo huku washiriki wakijipatia fursa mbalimbali ikiwemo mshindi wa kwanza kujishindia gari.
Washiriki wa shindano hilo wamesema wamejiandaa vyema na bado wanaendelea kujinoa zaidi ili kuhakikisha atakayeibuka mshindi anaiwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano ya dunia huku wakielezea furaha yao kubwa kwa mashindano hayo kufanyika Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza.
Kamati ya Miss Tanzania 2016 ambapo kutoka kulia ni Hashim Lundenga, Pamela Irengo, Flora Lauwo.
Mkutano baina ya Kamati ya Miss Tanzania 2016 na Wanahabari Jijini Mwanza
Washiriki wa Miss Tanzania 2016 katika ubora wao

 JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S4.

Kwa wale wanaopenda ku-flash simu zao na kuzipa muonekano wa ukweli basi watakuwa wameshasikia kuhusiana na custom recovery. Custom Recovery ni njia ambayo itakuwezesha kutumia custom rom kwenye simu.

Leo tutaongelea jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy S4 (GT-I9500). 
Jina la custom recovery ambayo tutaweka kwenye S4 (GT-I9500) ni PHILZ TOUCH RECOVERY.

Kujua aina ya recovery ambayo imekuja na samsung galaxy S4 unatakiwa kuizima simu yako kisha Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano na utaona recovery ambayo huwa inakuja na simu yako. Sasa sisi tunachofanya ni kuitoa hiyo iliyokuja na simu na kuweka PHILZ TOUCH RECOVERY. ambayo ina uwezo mkubwa  

Kabla sijatoa malekezo jinsi ya kuweka Philz Touch Recovery kwenye S4 (GT-I9500) ni vyema kukupa vigezo vya kuzingatia kabla ujajaribu kuweka custom recovery kwenye S4.

(VIGEZO NA MASHARTI)

1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.
2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer
3: Maelekezo haya ni kwa watu wanaotumia SAMSUNG GALAXY S4 (GT-I9500).
4: You need common sense and brain.
5: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window
6: Install Samsung kies kwenye compuer yako ili kupata drivers za samsung galaxy S4. Samsung Kies inapatikana HAPA. Hakikisha unadownload kies na sio kies3

MAELEKEZO YA KUWEKA PHILZ TOUCH RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S4 GT-I9500

STEP 0
 Hakikisha kama simu yako ni model GT-I9500. Kama ni tofauti na hiyo tafadhali usiendelee unaweza ukaharibu simu yako. 

 STEP 1
 Download Odin program zip file kwenye computer yako  DOWNLOAD
Jina la file ni Odin3 v3.09.zip 

STEP 2
 Download Philz Touch Tar file kwenye computer yako  DOWNLOAD
Hakikisha jina la file utakalo download ni philz_touch_6.41.6-i9500.tar.md5
Likimaliza kujidownload likopi na uliweke kwenye desktop ya computer yako

 STEP 3
Unakumbuka lile file ulilo-download kwenye step1 (Odin zip file,  Odin3 v3.09.zip)? sasa lifungue (Extract/Unzip) kwenye computer yako kwa kutumia (7-zip free software,  au Win Rar) ili upate hili file.Odin3 v3.09.exe kisha liweke kwenye desktop pamoja na lile file ambalo umelidownload kwenye step 2 ambalo ni philz_touch_6.41.6-i9500.tar.md5

STEP 4 
Double-click the Odin3 v3.09.exe file to open Odin

STEP 5 
Izime simu yako kisha subiri kama sekunde 10.Washa simu yako ya samsung galaxy S4 kwenye download mode. Tazama picha chini kisha soma maelekezo chini ya picha kujua jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode

 Jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode bonyeza kitufe cha katikati (Home) + cha kupunguza sauti (Volume down) + na cha kuwashia (power) kisha vishikilie kwa pamoja mpaka utakapoana kwenye screen yako maneno yanayosema Press Volume Up now to continue to Download Mode. Sasa achia halafu bonyeza cha kuongeza sauti. (Volume up)

Hakikisha simu yako inamuonako kama picha ya kulia inavyoonyesha chini kabla ujaendele  kwenye step 6.

 STEP 6 
 Kwenye computer yako hakikisha uko kwenye ile Odin program ambayo uli double click kwenye step 4.  Sasa chomeka simu kwenye computer ikiwa bado kwenye download mode kwakutumia usb cable. Odin itaitambua simu yako na itaonyesha message kama inavyoonekana kwenye picha chini
 
STEP 7
Kwenye Odin Click  AP button na chagua lile file ambalo uli download kwenye step 2 ambalo uliliweka kwenye desktop. Jina la file ni philz_touch_6.41.6-i9500.tar.md5

Muekano wako kwenye computer utakuwa hivi endapo utakuwa umenifwatilia vizuri. Tafadhali naomba Odin yako kwenye computer iwe na muonekano kama huo. Viboksi ambavyo vinatakiwa viwe na alama ya vema ni Auto Reboot na F.Reset Time kama inavyoonekana kwenye picha.

STEP 8 
Kabla ya kuendelea hakikisha tupo pamoja. Usiendele kama ujaelewa. 

STEP 9
Kwenye Odin bonyeza start button ambayo ipo chini kabisa kisha subiri mpaka utakapoana Odin imekuandikia PASS kama picha inavyoonyesha chini. Chomoa simu yako kwenye computer kisha subiri mpaka itakapowaka yenyewe kama ikichelewa kuwaka basi bonyeza cha kuwashia na itawaka kama kawaida.

 STEP 10
 Hongera mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako ya galaxy S4 (GT-I9500) na utakuwa na uwezo wa kuflash rom mbalimbali ili kupata muonekano mzuri na kuongeza ufanisi zaidi. 

Ili kuhakikisha simu yako ina custom recovery basi zima simu yako kisha subiri kama sekunde kumi. Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) kwa sekunde kama tano. Endapo utafanikiwa basi simu yako itakuwa na muonekano ambao unafana na picha inavyoonyesha chini. 

Jumamosi, 29 Oktoba 2016

UCHAMBUZI WA SHERIA ZA MAKOSA MTANDAO, 2015

Awali ya yote nirudie kutoa pongezi kwa serikali kwa hatua hii muhimu waliyofikia ya kuwasilisha mswada wa sheria mtandao ambao naimani kubwa itakua na majibu mazuri ya kudhibiti na kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao nchini. Naomba itambulike Tanznaia si ya kwanza kuwa na sheria za usalama mitandao na ukweli ni kwamba tumechelewa kwa kiasi Fulani. Nchi nyingi tayari zinasheria za usalama mitandao na zimeendelea kuboreshwa kadri teknolojia inavyo endelea kukua na kubadilika.

Nitaanza na mifano michache kunasheria mitandao zilizopendekeza kifungo cha maisha kwa wahalifu mtandao nchini Uingereza. Na katika Kikao cha usalama mitandao kilichopita mshiriki aliyekua nami meza kuu katika kuongoza moja ya kikao aliyetokea “US Secret service” alipata kuainisha adhabu ya miaka kumi na sita bado imeonekana ni ndogo na inashauriwa kuongezwa makali.

Aidha, Nieleze ushauri wa kuhakiki sheria mitandao zinaboreshwa na kuwa kali zaidi ni kutokana na athari ya uhalifu mtandao kua kubwa sana na imekua ikimgusa kila mmoja wetu – Kwan nje ya nchi kila siku tumekua tukipata habari mpya ya matukio ya kiuhalifu mtandao ambapo maelfu wamekua wakipoteza maisha, fedha na pia ufaragha wao umekua ukitumiwa vibaya na wahalifu mtandao.

Tanzania pia hatuko salama – Nimekua nikipata malalamiko mengi ya watu kudukuliwa faragha zao, kuibiwa fedha nyingi sana na wengine kufikia hata kujitoa maisha kwa kudalilisha mitandaoni.

Hayo yote yamekua yakisukuma wataalam usalama mitandao kuumiza vichwa kuhakiki wanakuja na mwarubaini wa uhalifu huu mtandao unaozidi kuota mbawa kila kukicha. Hapo ndipo mengi yakawekwa sawa katika kukabiliana na hali hii ikiwa ni pamoja na kukuza uelewa kwa watumiaji mtandao (Matumizi salama ya mitandao), Kuzalisha na kuongezea uwezo kwa wataalam wa usalama mitandao, kuwa na sharia stahiki za uhalifu mitandao, kukuza ushirikiano kutokana na uhalifu huu kutokua na mipaka, kuhimiza kupatikana kwa takwimu sahihi za uhalifu mitandao ili kuweza kutambua maeneo athirika zaidi.

Kwenye hili la Sheria ni hatua nzuri sana ambapo Tanzania imefikia ili kuweza kurahisisha mapambano dhidi ya uhalifu mtandao nchini na kuhakiki taifa linabaki salama kimtandao. Naimani Kila mmoja wetu ukizingatia wote ni wahanga kwa namna moja au nyingine ya uhalifu mtandao lazima tufurahie na kulipokea hili kwa mikono miwili. Wataalam wa usalama mitandao wamefurahishwa sana na hatua hii yetu na pongezi ni nyingi sana hadi sasa.

Kuondoa hofu Watanzania naomba nieleze kwamba katika kuandaa muswada huu wataalam na wadau mbali mbali walishirikishwa na badae kuvuka mipaka kwa wataalam kutoka mataifa mbali mbali katika maswala haya ya usalama mitandao kutoa maoni yao na kuboresha – Haikukomea hapo imepitia hatua kadhaa na hata kupelekea kauli yangu niliyo itoa katika moja ya vikao vya wataalam wa usalama mitandao kueleza kuwa “ Hatua za kitaalam zimekwisha sasa ipo kwenye hatua za kisiasa kuweza kupatiwa Baraka kabla ya kuwasilishwa bungeni” – Kauli ambayo wataalam waliona taifa letu linachelewa sana kwani sharia zilikua hazina shaka na hata kupitiwa kwakwe kulipaswa kua kwa muda mfupi.

Nimepata kufatilia kwa karibu kinachozungumzwa na wengi, Hofu kubwa nilizo ziona ambazo nimeona nizitole ufafanuzi ni kama ifuatavyo: -

MOJA, hofu kuwa uchunguzi wa makosa haya inaweza ikawa inakiuka faragha. Naomba nieleze kuna anaefahamu faragha yake iko dhaifu kiasi gani mara tu anavyo kua mtandaoni? Ni wazi kabisa unapaswa kujua faragha haiingi matatani tu kwa sababu ya sharia hizi mtandao.

Uchunguzi wowote wa uhalifu mitandao duniani kote unahusisha uangalizi wa kina hatua kwa hatua kwa kila ushaidi wa kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupitia kwa karibu kila chembe ya shaka ya kile kinachoweza kuonekana kinaweza kuwa na chembe ya sababu ya uhalifu mtandao.

Uchunguzi wa makosa ya digitali ni fani na ina maadili yake – Maadili ambayo yanasomewa darasani. Maadili hayo yana hakiki mchunguzi anafata masharti na vigezo stahiki vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kutotoa siri zisizoendana na uhalifu mtandao unaochunguzwa pamoja na kuwasilisha ushahidi kwa mhusika pekee bila kushirikisha kila mtu. Zaidi inawatu maalum si kila mtu anatakiwa kushiriki katika uchunguzi wa uhalifu mtandao. Na hili kuna moja ya masharti yana sisitiza kushirikisha idadi ndogo sana ya wachunguzi ni vyema zaidi.

MBILI, kuna hofu kwanini makosa mtandao yanapatiwa ruhusa ya kuchunguzwa bila hata kusubiri ruhusa ya mahakama? Ikumbukwe kuwa kwanza uhalifu mtandao unafanyika kwa haraka sana na hauna mipaka. Ndio maana hili limeangaliwa sana na kuamua kutoa ruhusa kwa wapelelezi teule wa makosa ya uhalifu mtandao kupewa fursa ya kuazisha uchunguzi mara moja bila ya kungoja mahakama, Ikumbukwe kuna kinachoitwa “search warrant” ambacho mchunguzi wa makosa mtandao anakua nacho nahii inatolewa na kiongozi katika kitengo kinacho jihusisha na usalama mitandao katika taifa husika. Kusisitiza hili kama pangetolewa ruhusa kusubiri protokali za mahakama kufatwa kumbuka uhalifu mtandao unauwezekano mkubwa sana wa kupotezwa ushaidi wake na kusababisha ugumu kwenye kufikia malengo.

TATU,Hofu ya faragha ya kupekuliwa mawasiliano – Niulize kama unatumia mtandao kuwasiliana vizuri hofu inatoka wapi kwenye hili. Kama unajua hunachembe ya uhalifu mtandao katika mawasiliano yako sidahani kuna haja ya kua na hofu kuchunguzwa. Na ikumbukwe yule aliyetiliwa mashaka pekee ndie anaye pekuliwa si kila mmoja atapekuliwa mawasiliano yake. Hii iko kila mahali duniani sisi sio wa kwanza.

Mimi nadhani hofu kubwa tulitakiwa kuwa nayo ni kuhusu mamilioni ya pesa yanayo potea katika mabenki yetu, athari za lugha za uchochezi kwenye mitandao, athari za kuporomoka kwa maadili yetu, athari za mama na dada zetu kusambazwa picha zao za uchi mitandaoni, athari za wasanii wetu kutopata mapato kutokana na watu kuiba kazi zao mitandaoni, athari za kudukuliwa na wahalifu mitandao na taarifa zetu kutumiwa vibaya, athari za kuogopa kufanya miamala ya kifedha kupitia simu zetu, athari za kuogopa kuweka pesa benki inayo pelekea uchumi wa taifa kuyumba, athari zilizombele yetu zinazoweza kupelekea kuhatarisha maisha ( Kufa) kupitia uhalifu mtandao na athari nyingine nyingi.

Ikumbukwe athari ni kubwa sana za uhalifu mtandao na hofu kubwa tulipaswa tuwe nayo na kwapamoja tuungane kuhakikisha sharia mtandao zinazidishwa makali na uchunguzi wake unafanywa kwa kina na utaalam wa hali ya juu. Hili ndilo linapelekea wataalam tunakutana mara kwa mara kuongezeana uwezo wa kuhakiki tuna tambua mbinu mpya za uhali mtandao na kujinoa kujua namna ya kuchunguza na kuweza kufikia malengo ya kudhibiti.

Wabunge walionyesha hisia zao kutaka kupata ufumbuzi wa mabilioni ya pesa yanayopotea katika mabenki na makampuni ya simu kupitia uhalifu mtandao – Wanapaswa kukumbuka udhibiti unapaswa kwenda sambamba na kua na sheria madhubuti zinazoweza kuhimili hali mbaya ya uhalifu mtandao nchini.

Naomba tu kusisitiza watanznaia kusoma na kuelewa na sio tu kufata mikumbo kwenye hili. Aidha, Hofu kubwa lazima iondoshe hofu ndogo. Nikiimanisha Uhalifu mtandao nitishio kubwa kuliko ugaidi na sheria zetu zanafanana kabisa na sheria nyingine za mataifa mbali mbali huku baadhi zikiwa kali zaidi kuliko tulizo nazo. Nimalizie kwa kutoa wito wa matumizi salama ya mitandao ili kujiepusha na kuingia matatani bila sababu za msingi. Huku nikiwatoa watanznaia hofu juu ya uchunguzi wa dhati wa makosa haya uanafanywa na hakuana atakae ingia matatani kama si muhusika.