UCHAMBUZI WA SHERIA ZA MAKOSA MTANDAO, 2015


Nitaanza na mifano michache kunasheria mitandao zilizopendekeza kifungo cha maisha kwa wahalifu mtandao nchini Uingereza. Na katika Kikao cha usalama mitandao kilichopita mshiriki aliyekua nami meza kuu katika kuongoza moja ya kikao aliyetokea “US Secret service” alipata kuainisha adhabu ya miaka kumi na sita bado imeonekana ni ndogo na inashauriwa kuongezwa makali.
Aidha, Nieleze ushauri wa kuhakiki sheria mitandao zinaboreshwa na kuwa kali zaidi ni kutokana na athari ya uhalifu mtandao kua kubwa sana na imekua ikimgusa kila mmoja wetu – Kwan nje ya nchi kila siku tumekua tukipata habari mpya ya matukio ya kiuhalifu mtandao ambapo maelfu wamekua wakipoteza maisha, fedha na pia ufaragha wao umekua ukitumiwa vibaya na wahalifu mtandao.
Tanzania pia hatuko salama – Nimekua nikipata malalamiko mengi ya watu kudukuliwa faragha zao, kuibiwa fedha nyingi sana na wengine kufikia hata kujitoa maisha kwa kudalilisha mitandaoni.
Hayo yote yamekua yakisukuma wataalam usalama mitandao kuumiza vichwa kuhakiki wanakuja na mwarubaini wa uhalifu huu mtandao unaozidi kuota mbawa kila kukicha. Hapo ndipo mengi yakawekwa sawa katika kukabiliana na hali hii ikiwa ni pamoja na kukuza uelewa kwa watumiaji mtandao (Matumizi salama ya mitandao), Kuzalisha na kuongezea uwezo kwa wataalam wa usalama mitandao, kuwa na sharia stahiki za uhalifu mitandao, kukuza ushirikiano kutokana na uhalifu huu kutokua na mipaka, kuhimiza kupatikana kwa takwimu sahihi za uhalifu mitandao ili kuweza kutambua maeneo athirika zaidi.
Kwenye hili la Sheria ni hatua nzuri sana ambapo Tanzania imefikia ili kuweza kurahisisha mapambano dhidi ya uhalifu mtandao nchini na kuhakiki taifa linabaki salama kimtandao. Naimani Kila mmoja wetu ukizingatia wote ni wahanga kwa namna moja au nyingine ya uhalifu mtandao lazima tufurahie na kulipokea hili kwa mikono miwili. Wataalam wa usalama mitandao wamefurahishwa sana na hatua hii yetu na pongezi ni nyingi sana hadi sasa.
Kuondoa hofu Watanzania naomba nieleze kwamba katika kuandaa muswada huu wataalam na wadau mbali mbali walishirikishwa na badae kuvuka mipaka kwa wataalam kutoka mataifa mbali mbali katika maswala haya ya usalama mitandao kutoa maoni yao na kuboresha – Haikukomea hapo imepitia hatua kadhaa na hata kupelekea kauli yangu niliyo itoa katika moja ya vikao vya wataalam wa usalama mitandao kueleza kuwa “ Hatua za kitaalam zimekwisha sasa ipo kwenye hatua za kisiasa kuweza kupatiwa Baraka kabla ya kuwasilishwa bungeni” – Kauli ambayo wataalam

Nimepata kufatilia kwa karibu kinachozungumzwa na wengi, Hofu kubwa nilizo ziona ambazo nimeona nizitole ufafanuzi ni kama ifuatavyo: -
MOJA, hofu kuwa uchunguzi wa makosa haya inaweza ikawa inakiuka faragha. Naomba nieleze kuna anaefahamu faragha yake iko dhaifu kiasi gani mara tu anavyo kua mtandaoni? Ni wazi kabisa unapaswa kujua faragha haiingi matatani tu kwa sababu ya sharia hizi mtandao.
Uchunguzi wowote wa uhalifu mitandao duniani kote unahusisha uangalizi wa kina hatua kwa hatua kwa kila ushaidi wa kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupitia kwa karibu kila chembe ya shaka ya kile kinachoweza kuonekana kinaweza kuwa na chembe ya sababu ya uhalifu mtandao.
Uchunguzi wa makosa ya digitali ni fani na ina maadili yake – Maadili ambayo yanasomewa darasani. Maadili hayo yana hakiki mchunguzi anafata masharti na vigezo stahiki vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kutotoa siri zisizoendana na uhalifu mtandao unaochunguzwa pamoja na kuwasilisha ushahidi kwa mhusika pekee bila kushirikisha kila mtu. Zaidi inawatu maalum si kila mtu anatakiwa kushiriki katika uchunguzi wa uhalifu mtandao. Na hili kuna moja ya masharti yana sisitiza kushirikisha idadi ndogo sana ya wachunguzi ni vyema zaidi.
MBILI, kuna hofu kwanini makosa mtandao yanapatiwa ruhusa ya kuchunguzwa bila hata kusubiri ruhusa ya mahakama? Ikumbukwe kuwa kwanza uhalifu mtandao unafanyika kwa haraka sana na hauna mipaka. Ndio maana hili limeangaliwa sana na kuamua kutoa ruhusa kwa wapelelezi teule wa makosa ya uhalifu mtandao kupewa fursa ya kuazisha uchunguzi mara moja bila ya kungoja mahakama, Ikumbukwe kuna kinachoitwa “search warrant” ambacho mchunguzi wa makosa mtandao anakua nacho nahii inatolewa na kiongozi katika kitengo kinacho jihusisha na usalama mitandao katika taifa husika. Kusisitiza hili kama pangetolewa ruhusa kusubiri protokali za mahakama kufatwa kumbuka uhalifu mtandao unauwezekano mkubwa sana wa kupotezwa ushaidi wake na kusababisha ugumu kwenye kufikia malengo.
TATU,Hofu ya faragha ya kupekuliwa mawasiliano – Niulize kama unatumia mtandao kuwasiliana vizuri hofu inatoka wapi kwenye hili. Kama unajua hunachembe ya uhalifu mtandao katika mawasiliano yako sidahani kuna haja ya kua na hofu kuchunguzwa. Na ikumbukwe yule aliyetiliwa mashaka pekee ndie anaye pekuliwa si kila mmoja atapekuliwa mawasiliano yake. Hii iko kila mahali duniani sisi sio wa kwanza.
Mimi nadhani hofu kubwa tulitakiwa kuwa nayo ni kuhusu mamilioni ya pesa yanayo potea katika mabenki yetu, athari za lugha za uchochezi kwenye mitandao, athari za kuporomoka kwa maadili yetu, athari za mama na dada zetu kusambazwa picha zao za uchi mitandaoni, athari za wasanii wetu kutopata mapato kutokana na watu kuiba kazi zao mitandaoni, athari za kudukuliwa na wahalifu mitandao na taarifa zetu kutumiwa vibaya, athari za kuogopa kufanya miamala ya kifedha kupitia simu zetu, athari za kuogopa kuweka pesa benki inayo pelekea uchumi wa taifa kuyumba, athari zilizombele yetu zinazoweza kupelekea kuhatarisha maisha ( Kufa) kupitia uhalifu mtandao na athari nyingine nyingi.
Ikumbukwe athari ni kubwa sana za uhalifu mtandao na hofu kubwa tulipaswa tuwe nayo na kwapamoja tuungane kuhakikisha sharia mtandao zinazidishwa makali na uchunguzi wake unafanywa kwa kina na utaalam wa hali ya juu. Hili ndilo linapelekea wataalam tunakutana mara kwa mara kuongezeana uwezo wa kuhakiki tuna tambua mbinu mpya za uhali mtandao na kujinoa kujua namna ya kuchunguza na kuweza kufikia malengo ya kudhibiti.
Wabunge walionyesha hisia zao kutaka kupata ufumbuzi wa mabilioni ya pesa yanayopotea katika mabenki na makampuni ya simu kupitia uhalifu mtandao – Wanapaswa kukumbuka udhibiti unapaswa kwenda sambamba na kua na sheria madhubuti zinazoweza kuhimili hali mbaya ya uhalifu mtandao nchini.
Naomba tu kusisitiza watanznaia kusoma na kuelewa na sio tu kufata mikumbo kwenye hili. Aidha, Hofu kubwa lazima iondoshe hofu ndogo. Nikiimanisha Uhalifu mtandao nitishio kubwa kuliko ugaidi na sheria zetu zanafanana kabisa na sheria nyingine za mataifa mbali mbali huku baadhi zikiwa kali zaidi kuliko tulizo nazo. Nimalizie kwa kutoa wito wa matumizi salama ya mitandao ili kujiepusha na kuingia matatani bila sababu za msingi. Huku nikiwatoa watanznaia hofu juu ya uchunguzi wa dhati wa makosa haya uanafanywa na hakuana atakae ingia matatani kama si muhusika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni