Microsoft yalipa faini ya $10,000 kutokana na kulazimisha Windows 10!
Microsoft walazimika kumlipa mwanamke mmoja faini ya $10,000 (zaidi ya Tsh milioni 20) baada ya kompyuta yake ku-upgrade kwenda Windows 10 bila mapenzi yake – na kibaya zaidi kompyuta hiyo kuanza kuzingua baada ya hapo.
Mahakama iliamuru kulipwa fedha hizo baada ya mwanamke huyo kushinda kesi, ingawa Microsoft walipanga kukuta rufaa ila waliamua kulipa kiasi hicho ili kuepusha gharama zaidi ambazo wangeendelea kuzipata kama wangeendelea na shughuli za kimahakama zaidi kwa kufungua rufaa.
Mwanamke huyo kutoka jiji la California nchini Marekani alisema hakuwahi ata kusikia kuhusu Windows 10 ila ghafla alipokuwa anafanya masasisho ya kawaida (updates) kompyuta yake iliyokuwa na Windows 7 ilisasisha (upgrade) OS yake kwenda Windows 10. Kompyuta hiyo anayoitumia kwa shughuli za kiofisi ilianza kufanya kazi vibaya sana na ata kuathiri shughuli zake na ndipo alipoamua kuchukua hatua ya kuwashitaki Microsoft.
Tangu mwezi Machi watumiaji wa programu endeshaji ijulikananayo kama Windows 7 na nyinginezo wamekuwa wakilalamika kuwa kompyuta zao zimekuwa zikiupgrade kwenda 10 Windows bila idhini ya mtumiaji kuruhusu/kukataa mpango huo. Hali hiyo imekuwa ikileta ghadhabu kwa watumiaji wa Windows.
Awali ilikuwa ni chaguo la mtumiaji kufanya maboresho(upgrade) kwenda Windows 10 lakini kwa miezi kadhaa sasa Microsoft wamefanya Windows 10 kuwa muhimu (recommended) kutumika kwenye kompyuta.
Tayari Microsoft wamesema wanachukua hatua zaidi kuepusha jambo la ‘upgrade’ kutokea bila chaguo la mtumiaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni