Alhamisi, 14 Julai 2016

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA COMPUTER

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA COMPUTER



Asante kwa kutembelea blog yangu. asante kwa kuungana nami kwenye darasa la leo. hili swali limeoulizwa na mmoja wa wafatiliaji wa masomo yangu kwamba akitaka kununua computer aangalie vitu gani? kiukweli kuna vitu vingi sana vya kuangalia kabla hujanunua computer(iwe desktop au laptop) iwe mpya au ya zamani. leo nitaongelea mambo makuu matatu ambayo ni muhimu sana kuyazingatia kabla hujanunua computer. yafuatayo ni mambo muhimu sana ya kuzingatia.

1. UKUBWA LA RAM
nendo ram ni kifup cha neno RANDOM ACCESS MEMORY. kazi kubwa ya RAM ni kuisaidia computer kufungua mafile na mafolder mbalimbali, pia hufihadhi taarifa kwa muda mfupi na taarifa hizi huwa zinafutika pale tu unapozima computer na kuwasha. ili computer iwe faster au iwe slow hutegemea sana ukubwa wa RAM. ndio maana RAM isipokuwepo kwenye computer yako haiwezi kuwaka, itaishia kuonesha charge inaingia lakini haiwaki.  kwahiyo unapotaka kununua computer hakikisha RAM inakuwa na ukubwa wa atleast 2GB

2. UKUBWA WA PROCESSOR
Processor ni kama ubongo wa computer yako, kitu chochote kinachofanyika kwenye computer processor ndio hufanya kazi hiyo. yan mfano unabonyeza herufi M na inatokea, kitendo hiki cha kubonyeza na kutokea huwa kinafanywa na PROCESSOR. kwa jina lingine processor huitwA CENTRAL PROCESSING UNIT. kwahiyo unapotaka kununua computer ni muhimu kuhakikisha processor yako inaukubwa kias, atleast kuanzia 2GB.

3. UKUBWA WA HARD DISK
hard diski ndio memory ya computer yako. humo ndio huhifadhiwa vitu vyote unavyoviweka kkwenye computer, mfano unapoweka mizki au movies au mafile yako yote huhifadhiwa kwenye HARD DISK, kwa kifupi huwa inaitwa HDD. ukubwa wa HDD HUTEGEMEANA NA MATUMIZI YA COMPUTER HUSIKA. kama unamatumizi makubwa nunua computer yenye HDD kubwa. na kinyme chake ni sahihi.

NB

yapo mambo mengi ya kuzingatia kabla hujanunua computer hayo niliyoelezea ndio muhim zaid na nirahisi kuyatambua, pia kama ni laptop ni vema ukajua charge inakaa masaa mangapi kabla hujaiununua.

ninaamini somo hili litakuwa msaada kwako ulieuliza pia kwa wasomaji wengine kwani wengi wamekuwa na tatzo kama hili asante.
ASANTE SANA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni